Mradi wa RIPAT-SUA, ambao untatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Shirika lisilo la kiserikali la RECODA (Research, Community and Organizational Development Associates) unawezesha wakulima Wilayani Mvomero na Manispaa ya Morogoro kutumia teknolojia mbalimbali za kilimo na ufugaji. Mradi huo ambao ni sehemu ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) kati ya SUA na RECODA ambayo yanasimamiwa na Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia, unatekelezwa kwa kufuata mfumo mpya wa ugani wa RIPAT (Rural Initiatives for Participatory Agricultural Transformation) au kwa Kiswahili Jitihada Shirikishi za Kuleta Mageuzi ya Kilimo Vijijini. Tar 29/6 hadi 2 Julai, wakulima waliojengewa uwezo na mradi huo waliadhimisha Siku ya Wakulima (Farmers’ Field Day) kwa nia ya kusambaza teknolojia wanazotumia kwa wakulima wengine. Maadhimisho hayo yaliyokusanya watu wasiopungua 600 yalifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mlali, Wilayani Mvomero.
Kwenye picha ya pamoja ni Mgeni Rasmi (wa nne toka kulia, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Eng. Emmanuel Kalobelo, Makamu wa Mkuu Chuo, SUA, Prof. Raphael Chibunda wa tatu toka kulia, akifuatiwa na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Bw. Michael Waluse na mwisho Mratibu wa mradi Dkt. E.T. Malisa; toka kushoto ni mwakilishi wa Rasi wa Ndaki CVMBS, Dkt. Luziga, Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii na Insia, Dkt. S.J. Kabote, na Mkulima wa Kata ya Magadu, Bw. Musa Muhidin)